Thursday, May 30, 2013

Bigg Brother:Tanzania yaanza kuonesha makucha Ammy Nando ndani ya Jakuzi moja na Dillish mrembo kutoka Namibia.Angalia Video hapa


Jana (May 29) ilikuwa ni usiku wa tatu katika jumba la big brother Afrika huko Afrika Kusini mengi yanazidi kuonekana na sasa washiriki wengi wanaanza kuonesha side B ya mioyo yao na kujaribu kupata muda wa kuwa romantic na kuonesha upendo (Romantic time). 

 Wakati washiriki wengine wakiendelea na mambo yao mtanzaniaAmmy Nando alijiachia kwenye bafu moja na na kuoga na mrembo Dillish kutoka na Namibia ambae ni mwanafunzi wa mwaka wa tatu akisomea Saikolojia.

Huenda huu ukawa mwanzo wa mahusiano yao humo ndani kwa sababu moyo hauna pazia na uzuri wa Dillish unaweza kumvuta to the limit model huyo wa kitanzania. 

 Kwa upande mwingine the boss lady toka Kenya Huddah Monroe alipata nafasi ya kushare na  Denzel mawili matatu hasa kuhusu mahusiano, wakati Denzel akiwa ameonesha tangu mwanzo kudata kwa Huddah. 



Jana Huddah alifunguka na kumwambia kuwa anahitaji mwanamme mwenye pesa na kwamba she is a gold digger.
 

Wiki hii Benzel, Betty, Huddah, Selly na Natasha wako katika nafasi ya  kukumbwa na Eviction

VIDEO  YAO: 

Finally:Matokeo ya kidato cha nne yatangazwa click hapa kuangalia.

http://www.necta.go.tz/matokeo_html_2013/CSEE_2012/olevel.htm

Friday, May 24, 2013

Chris Brown a.k.a Breezy apokea simu ya vitisho baada ya kuchora Graphic ya kutisha nje ya ukuta wake

Muimbaji Chris Brown amejikuta aki ‘spend’ weekend yake akiwa
katika hali ya wasiwasi baada ya kupata vitisho vya kumuondoa uhai
kutoka kwa watu wasiofahamika.

Kwa mujibu wa vyanzo, mwanasheria wa Chris, Mark Geragos
 alipokea simu kutoka kwa watu tofauti wasiojulikana 
wakitishia kumuua Chris Brown bila kutoa sababu. Baada
 ya vitisho hivyo Geragos aliamua kutoa taarifa idara ya 
polisi ya Los Angeles ambao wanaendelea kufanya upelelezi
 juu ya vitisho hivyo.
Hivi karibuni Chris Brown amekosa maelewano mazuri na 
majirani zake kutokana na wao kutofurahishwa na graffiti ya 
Chris aliyoichora nje ya uzio ya nyumba yake ya Hollywood 
Hills kwa madai kwamba kuna watoto wadogo ambao wanaishi
 na kupita eneo hilo ambao wanatishika na michoro hiyo yenye muonekano unaotisha, kitu ambacho kinahisiwa kuwa kinaweza kuwa
 moja ya sababu za vitisho alivyovipata.

UHURU KENYATTA KUTUMIA CHOPPER KUPUNGUZA FOLENI


Tangu Uhuru Kenyatta aingie madarakani uongozi wake umekuwa uki make headline kila siku kwa mambo ambayo pengine hayajawahi kufanyika
ali make headline kwa kuweka idadi ndogo kabisa ya mawaziri pia Makamu wake Bwana Ruto kununuliwa Private Jet ya kifahari kwa ajili ya mizunguko yake ya kikazi
sasa basi ishu mpya ni kwamba ametangaza kutumia chopper la kijeshi{pichani} itakayokuwa ikimtoa ikulu mpaka Airport ikisemekana kuwa nia ni kuondoa foleni itakayokuwa ikisababishwa na msafala wake endapo atatumia magari..
Unauonaje utaratibu huu??

PARIS HILTON ATUA NDANI YA CASH MONEY RECORDS



 
Baada ya Busta Rhymes, Drake, Nicki Minaj, Birdman, Lil Wayne sasa ni zamu ya Paris Hilton kutia timu ndani ya familia ya Cash Money.
mwanadada huyo ambae amegeukia kwenye mziki amesainiwa katika chama hilo kubwa kama ilivyoripotiwa na Rap-Up.com.
habari zinasema kuwa mwanadada huyu ambae ana mafanikio sana katika biashara zake ana record album yake ya pili kwa sasa ambayo itasimamiwa na Cash Money ambayo itahusisha wasanii wengi wa hiphop kama Lil Wayne.
jina la album hiyo bado haijatangazwa ila ya kwanza iliyotoka 2006 ilikuwa inaitwa Paris.

Kua wa kwanza kuangalia Fast and Furious 6 iliokua ikisubiriwa saana na mashabiki


Movie iliyokuwa inasubiriwa sana na mashabiki wa fast and furious 1,2,3,4 na 5, leo hii inatoka katika kumbi za cinema mbali mbali duniani kote ikiwemo na Tanzania, ambapo Fast and Furious 6 itaonyeshwa leo hii ndani ya ukumbi wa Century Cinemax kuanzia saa moja na nusu usiku. Cheki na treillar yake hapa kama hujawahi kuiangalia

Kijana aliekua akikabiliwa na kesi ya kula nyama za watu na kukutwa na kichwa cha Binaadamu AACHIWA HURU!!


 
Mahakama kuu kanda ya Dar es Salaam imeamua kumuachia huru Ramadhani Selemani Mussa ambaye alikuwa akikabiliwa na kesi ya kukutwa na kichwa cha mtu. Rama, ambaye muda wote huo alikuwa rumande gereza la Segerea akisota kusubiri hukumu yake, alikamatwa hospitali ya Muhimbili mwaka 2008 ambapo pia alikiri kuwa alikuwa na tabia ya kula nyama za watu ambayo amefundishwa kichawi toka alipokuwa mdogo. Mahakama imemuachia huru kwasababu mtuhumiwa alitenda kosa hilo pasipo kuwa na akili timamu. Hata hivyo mahakama hiyo imetoa agizo la kuendelea kumuweka kijana huyo katika hospitali ya wagonjwa wenye matatizo ya akili, hospitali ya Isanga iliyopo Dodoma mpaka pale atakapona ndipo aruhusiwe kurudi mtaaani.

SEASON YA NANE YA BIG BROTHER KUANZA WEEKEND HII


Siku ya tarehe 26 mwezi huu, itaanza kuonyeshwa rasmi msimu mpya wa big brother "the chase" kwa wale wenye dstv usikose kuangalia kupitia channel 198 upate kujua ni nani atakaeiwakilisha Tanzania mwaka huu. Dola laki tatu kushindaniwa 

SpankingNew!!the new Fast and Furious6 is now released with the Brand new Ludacris mixtape


Rapper LudaCris amedondosha moxtape yake mpya leo kupitia Datpiff.com ikiwa ni siku moja na release ya movie aliyoshiriki 'fast and furious 6', mixtape hiyo ina nyimbo10 na tayari ishadondoka leo hii, pichani ni cover yenye track list ya nyimbo hizo.

Thursday, May 23, 2013

MTWARA hali bado ni mbaya tazama hali ilivyo jioni hii!!


Mwandishi wetu aliyepo Mtwara ametueleza kuwa hivi sasa baadhi ya wananchi wa eneo la magomeni mkoani mtwara wamekimbilia katika Hospitali ya Mkoa wa Mtwara Lugula wakihofia usalama waokutokana na vurugu za kuchomwa kwa nyumba zao pamoja na vibanda vya biashara zilizotokea leo asubuhi katika eneo hilo..

Maduka maeneo ya Magomeni yamechomwa moto ikiwamo pia mali za Askari magereza . Mwanafunzi wa CHUNO amefikishwa hospitali Ligula na majeraha ya risasi mguuni.  
Mwanamke mwingine anayekadiriwa kuwa na miaka 25 mjamzito ameuawa kwa kupigwa risasi maiti ipo Ligula.




Kwa sasa( jioni  hii)  inaelezwa kuwa katika baadhi ya mitaa hali imetulia na ni idadi ndogo ya wananchi ndiyo inayoonekana wakitembea mitaani isipokua eneo la magomeni ambako mbomu yanaendelea kusikika huku huduma za kijamii katika mji huo zikiwa zimesimama zikiwemo usafiri, huduma za kibenki na shule

Hatimae Rais wa Jamhuri ya muungano Dk J.M.Kikwete atoa Amri ya kuwasaka wahusika Wakuu wa matukio yanayoendelea MTWARA "click hapa kutazama video"






WAKATI hali ikizidi kuwa tetea Mkaoni Mtwara kufutia Mapigano yaliyoanza jana Mkoani humo Rais Kikwete amevunja ukimwa wake na kutoa amri  wahusika wakuu wa tukio hilo kusakwa mara moja.


Akizungumza katika eneo la Kizota, Dodoma wakati wa kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Barabara ya Dodoma kwenda Iringa, Rais Kikwete  alisema wote waliohusika na vurugu hizo watasakwa na kuchukuliwa hatua kali.


Rais Kikwete alisema rasilimali inayopatikana mahali popote pale nchini inatakiwa kutumiwa na Watanzania wote... “Hivi watu wa  Nyarugusu wadai dhahabu ya pale au kinachopatikana Chalinze basi kisitumiwe na watu wa Morogoro! Hivi tutakuwa na taifa kweli?,”  alihoji kwa ukali Rais Kikwete.


Rais Kikwete alisisitiza kuwa Serikali itawasaka wale wote wanaoongoza vurugu hizo na watawajibishwa kwa makosa hayo..“Tutawasaka  .hawa watu na viongozi wao hata kama wana mapembe kiasi gani, tutayakata.
 

Kwa upande wake Waziri Muhongo Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo akisoma taarifa ya mapato na matumizi ya Wizara yake alisema mradi wa kusafirisha gesi kutoka mkoani Mtwara kwenda Dar es Salaam,  umeanza kwa kasina Waziri Mkuu, Mizengo Pinda atakwenda huko wiki ijayo kuweka jiwe la msingi.  

Akiwasilisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini jana, Waziri Muhongo alisema:
 

“Mradi wa kujenga bomba la gesi uko palepale na unaendelea kwa kasi na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda ataenda kuweka jiwe la msingi wiki  lijalo.”  

“Tumezungumza mengi kuhusu suala hilo na hata viongozi wa watu wa Mtwara walipelekwa nje kujifunza faida zake, lakini hata kama  hawajaelewa, nimetoa kijitabu kinachozungumzia faida mbalimbali watakazopata wana Mtwara katika mradi huo."
VIDEO:

Wanafunzi 25 wa shule ya sekondari Mwimbi waswekwa mahabusu!

WANAFUNZI 25 wa Shule ya Sekondari Mwimbi Kata ya Mwimbi wanashikiliwa na Polisi wilayani Kalambo mkoani Rukwa, wakituhumiwa kuteketeza kwa moto nyumba ya mkuu wao wa shule.

ZANZIBAR TENA....SHEHA WA TOMONDO- ZANZIBAR AMWAGIWA TINDIKALI JANA USIKU


\
Sheha Mohammed Omary Said aliyemwagiwa tindikali na mtu asiyejulikana akiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja Unguja akipatiwa matibabu, Sheikh Mohammed amepata maumivu makali sehemu za kifuwa na jicho kuumia

Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Mjini Magharibi,Mukhadam Khamis,amesema chombo kilichotumika kumwagia tindikali Sheha huyo kilipatikana eneo la tukio na kwamba polisi imekichukua kwa kukichunguza kitaalam ili kugundua aliyekuwa akikitumia kwa kuangalia alama za vidole.

Sheha huyo alimwagiwa tindikali jana usiku wakati alipotoka nje ya nyumba yake kuchota maji na ndipo mhalifu huyo alipomwagia tindikali na kwamba hakuweza kumtambua.

Sheha Mohammed Kidevu akiwa katika wodi ya Hospitali kuu ya Rufaa Mnazi Mmoja akipata matibabu ya majaraha ya kitu kinachosadikiwa kwa Tindi Kali,akipata matibabu hayo katika hospitali hiyo.

checkout12 great live performance in Billboard 2013 Music Awards


Watch 12 videos below

Bruno Mars ‘Treasure’
Macklemore & Ryan Lewis – ‘Thrift Shop’

Chris Brown – ‘Fine China’
Justin Bieber – ‘Take You’

Nicki Minaj & Lil Wayne – ‘High School’

will.i.am & Justin Bieber – ‘That Power’
Pitbull & Christina Aguilera – ‘Feel This Moment’
Ed Sheeran
Selena Gomez
Taylor Swift
Kacey Musgraves

MAJAMBAZI YAVAMIA GARI NA KUPORA FEDHA JIJINI DAR, TAZAMA PICHA ZA ENEO LA TUKIO HAPA


Matundu matatu ya risasi katika kioo cha gari lililovamiwa na majambazi.
Wanausalama barabarani wakichukua taarifa eneo la tukio.
Gari aina ya Toyota Vitz lililovamiwa na majambazi.
Wananchi wakiwa eneo la tukio.
Trafiki akielezea jambo baada ya tukio hilo.
Baadhi ya wananchi waliokusanyika kushuhudia tukio hilo.
Majambazi yaliyokuwa na silaha aina ya SMG yakiwa na pikipiki aina ya Bajaj Boxer yamevamia gari ndogo aina ya Toyota Vitz yenye namba za usajili T 929 CCX na kuwajeruhi watu wawili wenye asili ya Asia waliokuwa ndani yake na kuwapora furushi la fedha ambazo mpaka sasa bado haijafahamika ni kiasi gani. Tukio hilo limetokea eneo la Sayansi-Kijitonyama jijini Dar es Salaam.

HAYA NDO YALIYOWAPATA ASKARI WALIOMBAMBIKIZIA KESI YA KUKUTWA NA FUVU RAIA


https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEhNykRpN3XrQCLPnH6ZWXdWuJnWJKGvzPKKsTmKFED-O1OIUC0aGNvYbz9IQElvj2J0AIro5mnhHEjFE58c6c1FYOTj8IGXYo_RSdE0NDfLtU7juhEqWRYZXPW3ZqFJJmljXUpqLbwR48I/s1600/FUVU.jpg 
ASKARI Polisi watatu kati yao wawili wenye cheo cha Sajini na mwingine Koplo wa Jeshi la Polisi mkoani Morogoro, wamefukuzwa kazi baada ya kufikishwa mahakama ya Kijeshi wakituhumiwa kushirikiana na raia kumbambikia mfanyabiashara fuvu la kichwa cha binadamu.
Wakati hayo yakijiri mkoani Morogoro, kwa upande wa Arusha, polisi aliyekufuzwa kazi hivi karibuni kwa tuhuma za kukutwa akisafirisha bangi magunia 18, ametoroka mikononi mwa polisi wakati akipekuliwa nyumbani kwake, nje kidogo ya Jiji la Arusha kabla ya kufikishwa mahakama ya kiraia.
Kwa upande wa askari wanaodaiwa kutumia fuvu kubambikia kesi, wamefikishwa katika mahakama ya kiraia, wakidaiwa kumbambikia mfanyabiashara Samson Mwita kwa kutumia fuvu wakitaka wapewe fedha suala hilo lisifikishwe polisi.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, aliwataja askari hao ni D 4807 Sajini Sadick, D 4344 Sajini Mohammed wote kutoka Kituo cha Polisi Dakawa, wilayani Mvomero na E 3861 Koplo Nula wa Kituo cha Polisi Dumila, wilayani Kilosa.
Askari hao walifikishwa mahakamani wakiwa na mshirika wao Rashid Ally au Sharifu Hassan (47) mkazi wa Mbagala, Dar es Salaam na kesi yao imepangwa kutajwa Juni 3, mwaka huu.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa akisimulia tukio hilo lilitokea Mei 7, mwaka huu saa 12 :30 asubuhi katika mtaa wa Mgudeni, Kata ya Dumila, wilayani Kilosa, alisema askari hao watatu na raia huyo walikula njama ya utapeli kwa kumbambikizia mfanyabiashara maarufu kwa jina la ‘Mula’, fuvu linalosadikiwa kuwa la kichwa cha binadamu.
Hata hivyo alisema, askari hao walijipangia wenyewe kazi bila ya idhini ya wakuu wao na kwa kushirikiana na raia huyo waliamua kufanya vitendo vinavyokwenda kinyume na maadili ya kazi ya kutaka kujipatia fedha kwa njia ya kubambikiza kosa mtu mwingine.
Hata hivyo alisema, uchunguzi bado unaendelea ili kubaini mtandao wa matapeli wanaoshirikiana na askari wa jeshi hilo na akawaomba wananchi kuendelea kushirikiana na Polisi kwa kutoa taarifa na kuwafichua wahalifu na askari wanaokwenda kinyume na utendaji wao wa kazi.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa askari hao walimwambia mfanyabiashara huyo awapatie Sh milioni 25 kumaliza suala hilo kitu ambacho Mwita alikipinga na kuwataka kulifikisha suala hilo Kituo Kikuu cha Polisi Morogoro.
Polisi wa Arusha Akizungumzia kutoroka kwa Koplo Edward aliyekamatwa mkoani Kilimanjaro akisafirisha bangi, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema baada ya kufikishwa mahakama ya kijeshi ilikuwa afikishwe katika mahakama ya kiraia kujibu mashitaka hayo.
Kamanda alisema alitoroka wakati akipekuliwa nyumbani kwake na Ofisa wa polisi aliyekuwa akisimamia upekuzi huo, Inspekta Isack Manoni anahojiwa kuhusiana na kadhia hiyo.
Edward akiwa na mwenzake mwenye namba G.2434 Pc George walikamatwa Mei 18 mwaka huu saa 5 maeneo ya Himo wakiwa na magunia 18 ndani ya gari la Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU) la Mkoa wa Arusha lenye namba za usajili PT 2025 Toyota Land Cruiser wakitoka Arusha kwenda Holili mpakani mwa Kenya.
Akizungumza na waandishi wa habari jana, Kamanda wa polisi wa Mkoa wa Arusha, Liberatus Sabas alisema askari hao walishafukuzwa kazi na hatua za kuwafikisha katika mahakama za kiraia zilikuwa zikiendelea kwa kosa la kufanya biashara haramu ya bangi.
Sabas alisema askari hao walipelekwa nyumbani kwao eneo la Mrombo nje kidogo ya jiji la Arusha, kwa ajili ya upekuzi ndipo Edward alitoroka na kuwakimbia polisi ambao hawakufanikiwa kumkamata.

RATIBA YA JAY Z NDIO HII HAPA.... KUPIGA SHOW DAR OCTOBA 4!!KAbAaanG!


Jay Z ametoa mlolongo wa shows zake
atakazopiga kwa wiki 7 kuizunguka dunia kwa
dhumuni la kuleta ufahamu juu ya tatizo la
maji. Tour hii ndefu itaanza Septemba 9 huko
Krakow, Poland. Jay Z atadondoka Dar na
atagonga show hiyo tarehe 4 Octoba pale
Diamond Jubilee. Na hii ndio list ndefu ya
tour ya Jay Z:-
Sept. 9: Krakow, Poland (Coca-Cola SW Live
Festival)
Sept. 10: Bratislava, Slovakia (Incheba)
Sept. 15: Amsterdam (Heineken Music Hall)
Sept. 16: Germany (TBA)
Sept. 18: Istanbul (Refresh the Venue)
Sept. 19: Athens (Olympic Arena)
Sept. 21: Manchester, England (Evening News
Arena)
Sept. 22: Glasgow (SECC)
Sept. 23: Birmingham, England (National
Indoor Arena)
Sept. 24: London (Wembley Arena)
Sept. 26: Dublin (the Point)
Sept. 27: London (Royal Albert Hall)
Sept. 29: Paris (Le Zenith)
Sept. 30: Milan (Fiera di Milano)
Oct. 2: Barcelona (Teatro Heineken)
Oct. 4: Dar es Salaam, Tanzania (Diamond
Jubilee)
Oct. 6: Accra, Ghana (Accra Conference
Center)
Oct. 7: Lagos, Nigeria (Ocean View)
Oct. 9: Luanda, Angola (Cine Karl Max)
Oct. 11: Cape Town, South Africa (Belleville
Velodrome)
Oct. 13: Durban, South Africa (ABSA Stadium
Outer Fields)
Oct. 14: Johannesburg (Coca Cola Dome)
Oct. 17: Hong Kong (TBA)
Oct. 18: Bangkok, Thailand (BEC Tero Hall)
Oct. 20: Seoul, Korea (Walker Hill Gayagum
Concert Hall)
Oct. 21: Taipei, Taiwan (Taipei Dome)
Oct. 23: Singapore, Singapore (Suntec City
Concert Hall)
Oct. 25: Sydney (Entertainment Centre)
Oct. 27: Brisbane, Australia (Entertainment
Centre)
Oct. 28: Melbourne (Rod Laver Arena)

Samsung sells more than 10 million Galaxy S4 smartphones


An event employee displays a Samsung
Electronics Co. Galaxy S4 smartphone at the
World IT Show 2013 in Seoul, South Korea, on
Tuesday, May 21, 2013. South Korea's Samsung
Electronics said on Thursday that global sales
of its latest flagship Galaxy smartphone had
topped 10 million units less than a month after
its debut. -- FILE PHOTO: BLOOMBERG
SEOUL (AFP) - South Korea's
Samsung Electronics said on
Thursday that global sales of its
latest flagship Galaxy
smartphone had topped 10
million units less than a month
after its debut.
A company statement said the
Galaxy S4 had already topped
the 10-million sales mark
worldwide following its April 26
launch. Its predecessor, the S3,
had taken 50 days to pass the
same threshold.
The world's top handset maker
hopes the S4 will expand its presence in high-
end markets in the United States and
elsewhere, and crowd out archrival Apple and
its iconic iPhone.
Unexpectedly strong pre-orders for the S4 led
some US mobile carriers to temporarily delay

NI AJABU LAKINI KWELI KUTANA NA MWANAMKE HUYU, AMBAYE ANAUWEZO WA KUZUNGUSHA MGUU WAKE NYUZI 180 BILA YA KUSIKIA MAUMIVU


Katika picha chini juu ni mwanamke
anayefahahamika kwa jina la Jeo O'Shea,
kutoka Marekani. Miaka miwili iliyopita
aligundulika na ugonjwa wa kansa ya mifupa,
ambayo ilikua imeharibu mfupa mmoja katika
goti lake la mguu wa kulia.
Mwaka 2011 alifanyiwa upasuaji na kuondoa
sehemu hiyo ya mfupa iliyokua imeathirika na
saratani, lakini baada ya upasuaji akaja
kugundua kua anauwezo wa kuzungusha mguu
wake kwa nyuzi 180 bila ya kusikia maumivu.
Tazama video yake hapa chini jinsi
anavyozungusha mguu huo

Spanking New!!:Muakilishi wa Tanzania ====>>BBA 'THE CHASE


jYeah pipzz, huyu ndio muwakilishi wetu wa
BBA 'THE CHASE
KILA LA KHEIR FEZZA KESSY
WATANZANIA TUPO PA1!!

Wednesday, May 22, 2013

Tetesi: Polisi wanne, raia kadhaa wauawa. Picha: Ofisi, ambulance zachomwa moto Vurugu za Mtwara


Ofisi zachomwa moto
Ofisi zachomwa moto


Magari ya manispaa nayo yachomwa moto
Magari ya manispaa nayo yachomwa moto


Ambulance nayo yachomwa moto
Ambulance nayo yachomwa moto


mtwara-vurugu

TAFADHALI TAMBUA: Habari hizi zinaripotiwa na baadhi ya wananchi walioko Mtwara. Hazijathibitishwa hivyo zitumie kama muongozo tu, na si kama habari za uhakika.

Hadi kufikia saa hii (3:00 pm) kuna taarifa kwamba ofisiza CCM (maeneo ya Mdenganamadi na Majengo) zimechomwa moto; askari wanne wameuawa pamoja na wananchi kadhaa. Wananchi wanatumia baruti za kulipulia samaki kuwalipua majengo na askari.Hatari iliyopo ni kuchomwa kwa jengo la ofisi za mkuu wa mkoa. Yote haya ni.
kupinga bomba la gesi kujengwa kuelekea DSM.

MWAMUZI WA AFRIKA KUSINI KUICHEZESHA STARS MOROCCO

Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu (FIFA) limemteua mwamuzi kutoka Afrika Kusini kuchezesha mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia, Kanda ya Afrika kati ya Tanzania (Taifa Stars) na wenyeji Morocco (Lions of the Atlas).
Mechi hiyo ya kundi C itachezwa Juni 8 mwaka huu jijini Marrakech, Morocco kwenye Uwanja wa Grand kuanzia saa 3 kamili usiku kwa saa za Morocco. Mwamuzi atakayechezesha mechi hiyo ni Fraser Daniel Bennett.
Bennett atasaidiwa na Thusi Zakhele Siwela pia wa Afrika Kusini, wakati mwamuzi msaidizi namba mbili atakuwa ni Marwa Range kutoka Kenya. Mwamuzi wa akiba (fourth official) ni Lwandile Mfiki wa Afrika Kusini.
Kamishna wa mechi hiyo ni Robert Mangollo-M’voulou wa Gabon wakati mtathimini wa waamuzi (referee assessor) ni Charles Masembe kutoka Uganda.
Taifa Stars ambayo iko chini ya Kocha Kim Poulsen, na ikidhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager tayari iko kambini katika hoteli ya Tansoma ikiendelea kujinoa kwa ajili ya mechi hiyo ambapo kabla itajipima na Sudan (Nile Crocodiles) Juni 2 mwaka huu jijini Addis Ababa, Ethiopia.
Ratiba ya mazoezi kwa timu hiyo ni kama ifuatavyo;
Mei 22                 Saa 10 jioni                             Uwanja wa Karume
Mei 23                 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni   Uwanja wa Karume
Mei 23                 Saa 10 jioni                             Uwanja wa Karume
Mei 25                 Saa 1 asubuhi na Saa 10 jioni     Uwanja wa Karume
Mei 26                 Saa 3 asubuhi                            Uwanja wa Karume

AZAM MARINE WALETA MELI MPYA KALI ILE MBAYA, INAITWA KILIMANJARO IV , ICHEKI HAPA

 Muonekano wa Kilimanjaro 4
KAMPUNI ya Azam Marine, inaleta boti mpya ya Kilimanjaro 4, ambayo inatarajiwa kuwasili nchini nchini, kuanzia mwishoni wa mwezi huu, ikiwa na uwezo wa kubeba abiria 700 na kutumia muda wa dakika 70 kwa safari moja ya kati ya Zanzibar na Dar es Salaam. Hii ni boti mpya kabisa katika muendelezo wa boti za Kilimanjaro, ambayo itakidhi mahitaji ya wasafiri wa eneo hili kwa kuwa inabeba sifa zote, ambazo ni Usalama, Kasi zaidi na Unadhifu. Kaa tayari kwa mzigo mpya kutoka Azam Marine.

MTWARA KUMEKUCHA- MABOMU YARINDIMA, CHEKI PICHA ZA KINACHOENDELEA HAPA

https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94727&d=1369210247 
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94726&d=1369210162 
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94725&d=1369210066 
https://www.jamiiforums.com/attachment.php?attachmentid=94724&d=1369209998 
 
Mabomu yanapigwa mfululizo maeneo ya Magomeni-Mtwara . Takriban mabomu 20 na ushee mpaka sasa. Na wanaendelea kupiga mabomu. Sasa hali si shwari kila eneo, wakionekana watu watatu wanaongea maongezi maaskari wanapiga mabomu. Mabavu yamechukua mkondo wake. Wananchi wamejifungia majumbani mwao. Chuki dhidi ya Polisi yaimarika. Polisi wanapiga mabomu bila mwelekeo. Magomeni na sokoni kimenuka, mabomu yanarushwa na wananchi wanakimbia ovyo.
Kituo  kimoja  cha habari  kinachorusha habari za bunge chazuia mawimbi yake kwa Mkoa wa Mtwara hivyo hakisikiki(Redio na TV). Na kimewanyima haki wananchi wa Mtwara ya kupata taarifa.(Hatimaye wamerejesha matangazo yao)

Waziri wa Nishati amesoma hotuba yake kwa hisia kali na mbwembwe. Mwishoni amesema bomba la gesi linajengwa kutoka Mtwara kwenda Dar.

Maduka yote yamefungwa, baa zimefungwa, hakuna huduma za usafiri, ofisi za serikali zimepwaya kimsingi hakuna lolote linalofanyika
Boda boda zinazoonekana maeneo ya Nkanaledi na abiria zinapigwa mawe.
Makachero nao wanajifanya madereva wa boda boda na Bajaji, Tax wengine wanatembea na magari ya Serikali